Mwanamke mmoja ambaye anaugua saratani ya matiti amejioa mwenyewe baada ya kusubiri mchumba kwa muda mrefu.
May Chen mwenye umri wa miaka 28 kutoka Taiwan ameambia BBC kwamba anaugua ugonjwa huo lakini hajakubali sababu hiyo kuhujumu ndoto yake ya kuolewa.
''Nimekuwa nikisubiri mtu kujitokeza na kusema kwamba angependa kufunga ndoa nami mbali na kupiga picha za harusi nami aliambia BBC .
Anasema kwamba wakati unapohisi kwamba huna miaka mingi ya kuishi huna budi kujifanyia maswala ambayo yamekuwa ndoto yako.
Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa.
Anasema kwamba anatumia habari yake kuwapa moyo wanaougua kwamba maisha sio mabaya sana.
''Mbali na maisha na kifo mambo mengine yote ni madogo''.
Anasema kwamba watu wengi wanaougua huwa na wasiwasi wataishi kwa muda gani na lini watafariki ama iwapo matibabu wanayopata yanafanya kazi.
''Lakini mimi nawashauri kwamba usiwe na wasiwasi kwa sababu hujui, kwa hivyo kwa nini usijiliwaze''?
chanzo:bbc.
Comments