
Mwanajeshi huyo aliuawa Alhamisi umbali wa takriban kilomita 64 magharibi mwa mji mkuu Mogadishu, katika mji wa Barii.
Wanajeshi
wa Marekani walikuwa wanawashauri na kuwasaidia wanajeshi wa Jeshi la
Taifa la Marekani wakati wa operesheni hiyo, jeshi la Marekani limesema.
Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa wanajeshi wengine wawili wa Marekani walijeruhiwa kwenye mapigano.
"Mwanajeshi
huyo alipigwa risasi alipokuwa kwenye operesheni ya kushauri na
kusaidia Jeshi la Taifa la Somalia. Wanajeshi wawili walijeruhiwa katika
kisa hicho.
Wawili hao wanapokea matibabu," msemaji wa jeshi la
Marekani Afrika (Africom) Robyn Mack ameambia AFP.
Rais wa
Marekani Donald Trump aliongeza majukumu ya kijeshi la jeshi la Marekani
dhidi ya al-Shabab majuzi na kuwapa fursa ya kushiriki kwenye
operesheni dhidi ya wanamgambo hao wa mtandao wa al-Qaeda.
Kuuawa
kwa Mmarekani huo kumetokea siku tatu pekee tangu mkuu mpya wa jopo
kazi la Marekani la kuangazia eneo la upembe wa Afrika Brigidia Jenerali
David J. Furness kuzuru Mogadishu.
Alisema "tumejitolea kufanya kazi na mataifa washirika kuisaidia Somalia kusimama kidete dhidi ya kundi hili la msimamo mkali."
Mwaka
1993, wanajeshi wa Marekani walipokuwa wanashiriki kijeshi Somalia,
wanajeshi 18 waliuawa mjini Mogadishu wakipigana na wanamgambo wa
kiukoo.
Kisa hicho kiliangaziwa katika kitabu na filamu ya 'Black Hawk
Down'.
Al-Shabab wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya taifa ya Somalia ambayo inaungwa mkono na jamii ya kimataifa.
chanzo:Bbc.
Comments