Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Siha mkoani Kilimanjaro zimeendelea kuleta madhara ikiwamo kuvunjika daraja la mto simba lililopo West Kilimanjaro ambalo ni kiunganishi cha njia ya Lemosho ,Wasendo na Londrosi ambazo ndizo njia kuu za kupita watalii wanaokwenda kupanda Mlima Kilimanjaro.
Kufuatia hali hiyo Meneja wa shamba la miti la West Kilimanjaro, Magesa Mabeco ameomba Serikali kujenga daraja hilo ili kurejesha mawasiliano na huduma nyingine muhimu ndani ya eneo hilo.
Amesema kuvunjika kwa daraja hilo kutakuwa na athari pia kwa Serikali kwa sababu watalii wanaokwenda kupanda Mlima Kilimanjaro watashindwa kupita.
''Hii ndiyo njia kuu ya watalii mbalimbali wanaokuja kupanda Mlima Kilimanjaro,”amesema.
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Onesmo Buswelu amesema kuwa Serikali imelichukua jambo hilo na italifikisha eneo husika ili liweze kufanyiwa kazi.
Comments