
Katika mahojiano hayo, alitetea kipindi chake cha miongo
mitatau kama rais wa Uganda na kuwashutumu wale wanaomuita dikteta,
akisema kuwa huenda amekuwa dikteta mzuri kwa sababu amekuwa
akichaguliwa na wananchi mara tano.
Alizungumzia kufungwa kwa
mwanaharakati Stella Nyanzi ambaye anazuiliwa kwa kumuita, ''makalio''
akisema kuwa hana haki ya kuwatusi wengine.
''Iwapo wewe ni
mwanaharakati na unafanya makosa ,kwa sababu katika kupigania haki za
binaadamu pia unafaa kuzungumzia haki za wengine, huwezi kuvunja haki za
wengine na kusema kuwa ni haki yako kuwatusi watu hapana.
Haki zinaenda
sambamba na majukumu, iwapo unajua chochte kuhusu demokrasi. Alikataa
kuingizwa katika mazungumzo ya vita vilivyokuwa katika jimbo la
magharibi la Kasese,ambapo vikosi vya usalama vilikabiuliana na walinzi
wa mfalme wa eneo hilo, mzozo uliowacha makumi kufariki na wengine wengi
kuuawa akisema kuwa ni swala ambalo linaangaziwa mahakamani''.
''Swala
hilo liko mahakamani na kulingana na mahakama, wakati kitu kinapokuwa
mahakamani sifai kuzungumzia. Mahakama itatuambia iwapo watu hao
walikamatwa kwa sababu fulani ama la''.
chanzo:Bbc.
Comments