Muhimbili yataka wasioridhishwa na huduma za uuguzi wao waseme.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), Profesa Lawrence Museru  amewataka wananchi kutoa taarifa iwapo hawajaridhika na huduma za wauguzi MNH.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani Tawi la Muhimbili (TANNA) yaliyofanyika hospitalini hapo leo, Profesa Museru amesema ni wajibu wa muuguzi kutoa huduma inayostahili kwa mgonjwa kwa kufuata sheria zilizowekwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uuguzi MNH, Agnes Mtawa amewakumbusha wauguzi kuhakikisha wanafuata sheria za uuguzi na kuhakikisha wanapata leseni rasmi za uuguzi kisheria.
Amesema lazima wahakikishe wanawahudumia wagonjwa wote bila upendeleo, kuhudumia mgonjwa bila kuangalia itikadi, udini wala tatizo lililosababisha mgonjwa kufikishwa hospitalini.
Kufanya kazi kwa pamoja na kuhakikisha wanatunza siri za wagonjwa.
chanzo:Mwananchi.

Comments