
Tukio hilo la kusikitisha limetokea huko Mwache alale Wilaya ya Magharibi A Unguja.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa mjini Magharib Kamishan msaidizi muandamizi wa Polisi Hassan Nassir Ali amesema Tukio hilo la kusikitisha limetokea baada ya mtoto huyo kulazimishwa kwenda chuoni na wazee wake hivyo alitoka kuelekea chuoni lakini hakufika na ndipo alirudi na kuingia chumbani kwake na kujinga kwa kutumia pazia.
Aidha kamanda huyo alitoa wito kwa wazazi na walezi “kuchunguza michezo wanayoangalia watoto wao kwenye TV kwani mtoto wa umri huo hawezi kuwa na fikri ya kujinyonga na kujitoa uhai wake, lakini hayo yote yametokana na kuiga mamba ndani ya TV”.
Mwili wa marehemu huyo umefanyiwa uchunguzi katika Hospitali kuu ya Mnazi mmoja na kukabidhiwa jamaa za kwa ajili ya mazishi.
chanzo:zanzibar24.
Comments