
Mtuhumiwa huyo ambae alikua akifanya kazi ya kibarua cha ujenzi ndani
ya nyumba anayoishi mtoto huyo na baada ya kumaliza alienda nyumbani
kwao ambapo alifatana na mtoto huyo na ndipo ilipofika akamuingiza
chumbani kwake na kumfanyia kitendo hicho cha kinyama.
Kamanda wa Polisi mkoa wa mjini Magharib Kamishna msaidizi
muandamizi Hassan Nasir Ali amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kusema kuwa mtu huyo ameshakamatwa na polisi na mara baada ya
kukamilika kwa upelelezi mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
chanzo:zanzibar24.
Comments