Mpango wa uzalishaji sukari waonyesha mafanikio.

Uzalishaji wa sukari kwenye viwanda vya sukari hapa nchini umeongezeka kufuatia kuwepo kwa mpango wa miaka mitano wa maendeleo ya sukari nchini ambao kwa sasa mpango huo uko katika mwaka wa pili.

Hayo yalisemwa leo (Jumanne)  mjini hapa na mwenyekiti wa mfuko wa maendeleo ya sukari nchini, Deo Lyatto kwenye mkutano wa wataalamu wa kilimo cha miwa na wadau wengine wa sukari kutoka viwanda vya sukari Afrika Mashariki ikiwemo taasisi ya utafiti wa kilimo cha miwa na chuo cha utafiti sukari. 
Lyatto amesema kuwa mpango huo umesaidia kuvuka lengo la uzalishaji wa sukari kutoka tani 317000 mwaka jana hadi kufikia tani 326000 kwa mwaka huu. 
Mwenyekiti huyo amesema kuwa pamoja na kuongeza uzalishaji lakini mpango huo unalengo la kuongeza masoko ya ndani na nje ya nchi kutokana na kuwa na sukari ya kutosha.
Hivyo Lyatto alisema kuwa katika mkutano huo wadau hao wataweza kujadiliana changamoto zinazokwambisha maendeleo ya sukari hapa nchini na kuzitafutia ufumbuzi. 
Aidha alisema kuwa sekta ya sukari inategemea sana wataalamu kuanzia kwenye kilimo cha miwa hadi viwandahasa katika kuongeza uzalishaji na ubora. 
Kwa upande wake meneja wa wakulima wa nje wa miwa Kilombero, Job Zahoro amesema kuwa wakulima wa nje wanakabiliwa na changamoto nyingi katika uzalishaji ikiwemo ya kukosa mitaji itakayosaidia kuongeza teknolojia ya kwenye kilimo. 
 chanzo:mwananchi.

Comments