Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel apandishwa kizimbani.

jamii Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel Bwana Do Manh Hung amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kuhujumu uchumi wa Nchi.

Mshtakiwa huyo aliunganishwa na washtakiwa wengine saba waliofikishwa Mahakamani hapo mapema Mwaka huu.

Wote kwa pamoja wanakabiliwa ma mashtaka kumi, kula njama. Kisimika mitambo ya mawasiliano bila kibali cha TCRA, kutoa nyaraka za uongo, kusababisha hasara ya milioni 459 kwa serikali ya Tanzania, kutumia mitambo ya mawasilino ambayo haijathibitishwa na namba za simu.


Mbali na Hong, washtakiwa wengine ni Dilshad Ahmed (36), Rohail Yaqoob(47), Khalid Mahmood (59), Ashfaq Ahmad (38), Muhamad Aneess(48), Imtiaz Ammar (33) wote raia wa Pakistan na Ramesh Kandasamy (36) raia wa Sri-Lanka.
chanzo: zanzibar24.

Comments