Naibu
Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa
bungeni leo amefunguka na kusema hakuna tafsiri ya mavazi ya kike au
kiume kwa kuwa mavazi hayo kama suruali yanavaliwa na watu wote wanaume
hata wanawake.
Masauni
alitoa ufafanuzi huo bungeni kufuatia Mbunge kutaka kujua serikali
inachukua hatua gani kwa baadhi ya wanaume ambao wamekuwa wakijipamba na
kujilemba kwa kuvaa nguo za kike.
"Ni
kweli kuna wanaume wanavaa mavazi ya kike hata wanawake pia wapo
wanavaa mavazi ya kiume, ila sidhani suala la mavazi kama lina tafsiri
kuwa vazi hili ni la kike tu na hili ni la kiume tu, nadhani suala hili
la Mbunge linahitaji ufafanuzi wake wa kina ili tujue yeye alikuwa
anamaanisha nini zaidi katika jambo hili" alisema Masauni
Mbali
na hilo Naibu Waziri huyo alitolea ufafanuzi malalamiko ambayo
yametolewa kuwa wapo baadhi ya wanawake huvuliwa hijabu zao na kusema si
kweli kwani polisi wanafanya kazi zao kwa weledi na kufuata sheria.
"Si
kweli kwamba wanawake wanavuliwa hijjabu na nikabu zao na polisi wa
kiume pindi wanapokaguliwa kwani polisi wanafanya kazi zao kwa kufuata
sheria na umakini mkubwa, ila kama wapo watu wanafanya hivyo niwaombe
wanawake wote pindi wanapofanyiwa hivyo wapeleke malalamiko yao kwenye
vyombo husika tutalifanyia kazi, natambua kule Zanzibar kuna changamoto
katika kufanya ukaguzi lakini hatukuona wanawake wakivuliwa mavazi yao" alisisitiza Masauni
chanzo:Mpekuziblog.
Comments