
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Haji Khamis
Haji amesema tukio hilo limetokea jana majira ya 2:30 usiku katika eneo la
Kizimbani.
Kamanda
Haji alitaja chanzo cha tukio hilo kuwa ni wivu wa mapenzi.
Alisema
kuwa, marehemu alijeruhiwa baada ya kuchomwa kisu na mkewe katika mguu wake wa
kushoto na kutokwa na damu nyingi ambayo ndio iliyosababisha kifo chake.
"Khadija
alikwenda nyumbani kwa mke mwenziwe alipokuweko mumewe (marehemu) na kutaka
kuzungumza nae, ambapo hapo waligombana na ndipo mwanamke huyo alipochukua
hatua ya kumchoma kisu mumewe", alisema Kamanda Haji.
Alisema
kuwa, mara baada ya kujeruhiwa alikimbizwa katika hospitali ya Wete kwa ajili
ya matibabu, ambapo ilipofika saa 9:00 usiku alifariki.
Kamanda
huyo alisema kuwa kwa sasa mtuhumiwa yuko chini ya ulinzi na upelelezi
utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
Hivyo
aliwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi mwao na badala yake
wafike katika vyombo husika kuripoti, iwapo kuna kosa la jinai liweze
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa
upande wao wananchi wa eneo hilo, walidai kuwa Khadija alitoka kwake na watoto
wake huku akiwa na kisu kwenda kumwita mumewe, ambapo walianza kugombana nje ya
nyumba ya mke mwenzake na ndipo alipopandwa na hasira na kumchoma kisu cha mguu
mumewe.
Comments