
Akiwasilisha Hutuba ya Makadirio ya mapato ya Mwaka wa Fedha 2017/18 katika ukumbiwa wa Baraza la wawakilishi huko Chukwani, Waziri wa Elimu na Mfunzo ya amali Zanzibar Riziki Pembe Juma amesema ubora huo wa elimu utajumuisha kuwajengea stadi wananfunzi katika ngazi zote za elimu .
Amesema kipaumbele cha pili ni kuengeza upatikanaji wa fursa za elimu kwa usawa katika ngazi zote za elimu na Mafunzo ya amali.
Aidha amesema katika kuvitekeleza Vipaumbele hivyo Wizara imekusudia kuwalipia ada za mitihani, wanafunzi wote wanaofanya mitihani yao ya taifa kwa ngazi ya elimu ya msingi na ya sekondari.
Hata hivyo amesema Wizara pia itafuta michango ya wazazi na serikali itaharamia elimu ya maandalizi na msingi kwa kuzipatia skuli na wanafunzi vifaa vya kufundishia ikiwemo vitabu ,Madaftari ya mahudhurio na kuwapatia chakula wanafunzi wa maandalizi.
chanzo:Zanzibar24.
Comments