
Alisema jitihada hizo zinatokana na janga kubwa lililowakumba
Wananchi katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Zanzibar baada ya
Makaazi yao kukumbwa na mafuriko mengine yakiharibika kabisa.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo alipofanya ziara ya siku Moja
Kisiwani Pemba kujionea hali halisi ya athari ya mvua za Masika
zilizopelekea mamia ya Wananchi kukosa makaazi baada ya nyumba zao
kubomoka na nyengine kufunikwa na vifusi vya udongo.
Balozi Seif alisema Timu ya Wataalamu na Viongozi Watendaji wa
Serikali wamepewa jukumu la kufanya Tathmini kwa kushirikiana na Wakuu
wa Mikoa na Wilaya zilizopata maafa ili kujua maeneo na wananchi
wanaopaswa kupewa kipaumbela katika kusaidiwa kuanza tena maisha yao
kama kawaida.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefarajika kuona Wananchi walio
wengi katika maeneo mbali mbali yaliyoathiriwa na Mvua za masika
kuonyesha mshikamano wao kwa kusaidiana katika kipindi hichi cha maafa.
Alisema mwendo huo ulioweka pembeni itikadi za Kisiasa unafaa
kuendelezwa katika vipindi vyote yanapotokea maafa au majanga na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwa pamoja nao katika
vipindi vyote.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliyefuatana na Ujumbe mzito wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wale wa Chama Tawala
alitembelea Ghala la kuhifadhi Karafuu la Shirika la Tifa la Biashara
Zanzibar { ZSTC} Mkoani kujionena hali halisi iliyojitokeza kwa kubomoka
kutokana na mmong’onyoko wa Ardhi.
Balozi Seif aliupongeza Uongozi wa ZSTC kwa uamuzi wake wa kuyawekea
Bima Majengo yake jambo ambalo litaipunguzia gharama za ujenzi mpya wa
Jengo hilo linalohifadhi Karafuu zote za Kisiwa cha 9emba kwa ajili ya
kusafirishwa nje ya Pemba.
Balozi Seif aliushauri Uongozi huo wa ZSTC kuhakikisha kwamba majengo
mapya wanayojenga yanazingatia kiwango kinachokubalika Kitaalamu ili
kujie9usha ma maafa yanayoweza kutokea ikiwemo mi9oromoko na Mafuriko ya
Mvua.
Nae Afisa Mdhamini wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar {ZSTC}
Pemba Nd. Abdullah Ali Ussi alisema mmong’onyoko wa ardhi uliosababishwa
na Mvua kubwa ulifukia Magunia Mia 527 zenye Tani 23.7 za Karafuu kavu
zilizokuwa zimehifadhiwa katika Ghala hilo.
Nd, Abdullah alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba
kati ya hayo Magunia 518 yenye Tani 23.3 yameweza kuokolewa na hadi sasa
Gunia 9 zenye ujazo wa Kilo 405 zikiwa na gharama ya shilingi Milioni
5.6 bado hazijapatikana.
Alisema gharama za kulerejesha tena ghala hilo katika hali yake ya
kawaida linahitaji kiasi cha shilingi Milioni 50,000,000/- ambazo
zitashughulikiwa na Shirika la Bima linaloendelea na utaratibu wa
kufanya thathmini ya hasara hiyo.
Mapema asubuhi Balozi Seif na ujumbe wake alitembelea Ghala la ZSTC
Mkoani, kuangalia nyumba zilizoathirika katika Kijiji cha Mbuyuni pamoja
na Kijiji cha Changaweni kujionea hali halisi ya Miti ilivyoharibika
kutokana na upepo mkali uliovuma na kuambatana na Mvua kubwa.
Balozi Seif pia akaangalia sehemu ya Bara bara iliyokatika kutokana
na mong’onyo katika Kijiji hicho cha Changaweni, kuwafariji Wananchi
wa Kijiji cha Mwambe ambao nyumba zao zipatazo 15 zimeharibika kutokana
na Mvua kubwa pamoja na kuifajiri Familia ya Mzee Ramadhan mohamed
aliyefiliwa na Mtoto wake aliyeangukiwa na Ukuta wa Madrasa.
Akiwapa pole Wananchi wa Vijiji vya Chonga na Vitongoji Balozi Seif
alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lazima itowe msaada katika
muda mfupi kulingana na mazingira yaliyojitokeza ili kuona maisha ya
Wananchi wake yanarejea kama kawaida.
Balozi Seif aliwatahadharisha Wananchi kujiepusha na utaratibu wa
kupenda kujenga makaazi yao ya kudumu katika maeneo hatarishi kama vile
sehemu za Milima.
Wakitoa shukrani zao Wananchi walioathirika na kadhia hiyo Kisiwani
Pemba wameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada
inazoendelea kuchukuwa ya kusaidia Wananchi wake wakati wanaoatwa na
majanga.
Bwana Othman Abdulrahman Mabrouk wa Kijiji cha Chonga alisema
Wananchi walio wengi wamefarajika kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba
mitihani wanayoipata inapunguza machungu.
Hata hivyo Bwana Abdulrahman kwa niaba ya Wananchi wenzake wameiomba
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufikiria njia za kuwasaidia mitaji
itakayowawezesha kurejesha matumaini yao ya Kimaisha baada ya fursa
walizokuwa nazo kuata mitihani ya mafuriko.
Naye Mmoja wa Vijana wa Kijiji hicho Nd. Suleiman Khamis Rashid
alisema io haja kwa Serikali kupitia Wizara inayoshughulikia Taaluma
kuangalia uwezekano wa kuwapatia mabuku na Vitabu Watoto walioathirika
na mafuriko hayo ambao vifaa vyao vyote vimekumbwa na Maji.
Nd. Suleiman alisema kwa sasa wanafunzi wengi licha ya kufungwa kwa
skuli kutokana na mafuriko hayo lakini pia wanashindwa kuendelea na
msomo hayo kwa vile hawana vitabu wala mabuku ya kuandikia.
Akizungumza katika Kikao cha majumuisho kilichofanyika katika Hoteli
ya Archipelaago Chake chake Pemba wakati wa Usiku Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif aliwaasa Wasimamizi wa Taasisi za Umma
kuhakikisha kwamba kero zinazowakumba Wananchi katika maeneo yao
wanazichukulia hatua zinazofaa.
Balozi Seif alisema yapo malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya
Wananchi wakiwalaumu Viongozi wa Taasisi kushindwa kuchukuwa hatua kwa
wakati na matokeo yake wanajikuta kupata hasara kutokana na uzembe wa
Viongozi hao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alivipongeza Vikosi vya Ulinzi
Kisiwani Pemba kwa umakini na umahiri waliouonyesha katika kuwasaidia
Wananchi mbali mbali wakati walipokumbwa na maafa hayo.
![]() |
Sehemu ya Bara bara iliyokatika leo subuhi kutokana na mong’onyo wa ardhi uliosababishwa na Mvuua kubwa zinazoendelea kunyesha katika Kijiji cha Changaweni Mkoa wa Kusini Pemba. |
![]() |
![]() |
![]() |
Mashamba ya Migomba yaliyopo katika Kijiji cha Changaweni Wilaya ya Mkoani yaliyokumbwa na Upepo mkali na kusababisha kukatika au kung’oka kabisa. |
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
13/5/2017.
chanzo:zanzibar24.
Comments