
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika mafunzo ya siku moja ya athari za mabadiliko ya tabianchi Mratibu wa Mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianch Zanzibar
ZACCA Soud Mohammed Juma amesema kutokana na utafiti uliofanyika Zanzibar kunauwezekano mkubwa wa kupoteza ardhi yake jambo linalisababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na kuharibu miundombinu pamoja na kupoteza eneo lake la kilimo.
Hata hivyo amesema hali ya toto zanzibar imeongezeka kutokana na hali hiyo serikali iyoneumuhumi kutilia mkazo suala hili kwa kutoa elimu zaidi kwa wananchi kuwacha kuchimba mchanga,kukata miti,kuvamia maeneo hatarishi kwani itapelekea athari kubwa kwa wananchi hasa wanyonge.
Aidha waandishi wa habari kwa nafasi zao wametakiwa kuelimisha umma juu ya mabadiliko ya tabianch na athari zake kwani kuna mifano hai imeanza kujitokeza ikiwemo upepo mkali ya kimbunga,Mafuriko,maji ya bahari kuvamia makaazi ya wananchi pamoja na maeneo ya kilimo.
Kwaupande wao baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo Amina Mchezo na Ali Abdallah wamesema licha ya jitihada zinazochukuliwa za kuwaelimishwa jamii kupitia vipindi mbalimbali katika vyombo vya habari tatizo kubwa ni ukosefu wa ajira hupelekea jamii kuvamia maeneo hatarishi kwa kufanya shughuli zao za maisha ili kujikimu ikiwemo ukataji wa kuni,uchomaji wa mikaa,uchimbaji wa mchanga lakini serikali ikiwasaidia vijana kuwa wezesha tatizo hilo litapungua.
chsanzo:Zanzibar24
Comments