
Katibu mkuu wa jumuia ya nchi za Amerika, OAS, Luiz Almagro amesema hatua hiyo haikubaliki na ni kinyume cha katiba.
Marekani
imesema kuwa bunge la katiba ni njama tu za kumfanya Maduro aendelee
kubaki madarakani huku Brazil nayo ikisema kuwa huo ni mpango wa kufanya
mapinduzi.
Bunge la Congress linalodhibitiwa na upinzani limepiga
kura kukataa bunge jipya la katiba, likisema kuwa halitaundwa bila wao
kuridhia.
Wakati hayo yakijiri, katika hatua nyingine waandamanaji kwa mara
nyingine wamejitokeza barabarani na kusababisha misururu mirefu ya
magari.
Wakati rais Maduro akiona kwamba hatua hii ni ya kuwavunja
nguvu wapinzani ambao amewashutumu kutaka kumpindua, hasimu wake
Henrique Capriles amesema hayo ni maneno ya serikali iliyoshindwa ambayo
inataka kukwepa kuitisha uchaguzi.
Amesema maandamano yataendelea.
chanzo:Bbc.
Comments