Lipumba amsifu Jecha kufuta matokeo Zanzibar.

Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,  amesema ni afadhali  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha aliyefuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar kuliko Maalim Seif aliyejitangazia matokeo.
Lipumba amesema, Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF alifanya kosa kubwa  kujitangazia matokeo.

Lipumba anaendelea na mahojiano ya moja kwa moja yanayorushwa na televisheni ya Clouds.
chanzo:Mwananchi.

Comments