Mtandao wa habari wa al Yaum al Sabi' wa
nchini Misri imemnukuu Faiz al Sarraj, Waziri Mkuu wa serikali ya umoja
wa kitaifa ya Libya akiwaambia waandishi wa habari mjini Tripoli
kwamba, kuna udharura wa kuondolewa vikwazo vya silaha ilivyowekewa nchi
yake ili vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo kama jeshi na polisi viweze
kulinda usalama wa nchi hiyo.
Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa
kitaifa ya Libya amesema, jeshi na polisi ya Libya inahitajia kujengwa
upya, kupewa silaha, mafunzo ya kijeshi na kubadilishana taarifa za
kijasusi.
Faez al Sarraj ameongeza kuwa, wananchi
wa Libya hivi sasa wanateseka kwa matatizo mengi kwani nchi yao tangu
miaka kadhaa nyuma imekumbwa na migogoro ya kisiasa, kiuchumi na
kiusalama.
chanzo: parstoday.
Comments