
Majaribio hayo yalifanyika kulingana na sheria na taratibu za vyombo
vya majini ambayo inavitaka vyombo vyote vya majini kufanyiwa majaribio
kabla ya kuanza kazi ili viweze kupatiwa cheti cha ubora “Seaworthiness
Certificate”.

Mkuu wa Vivuko Magogoni/Kigamboni, Mhandisi Lukombe King’ombe
alisifu uwezo wa kivuko hicho na kuwataka wakazi wa maeneo hayo
kuhakikisha wanakitunza kivuko hicho kwani kitawasaidia kupunguza
msongamano wa abiria na magari hasa majira ya asubuhi na jioni.
Ujenzi wa MV KAZI ambacho kina uwezo wa kubeba abiria 800 magari 22
sawa na jumla ya tani 170. umegharimu jumla ya Shilingi Bilioni 7.3 za
Kitanzania.

chanzo:zanzibar24.
Comments