
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Zanzibar Kaimu waziri wa
afya Riziki Pembe Juma amesema maeneo yalijitokeza kuwepo na vimelea
hivyo ni pamoja na maeneo ya wilaya ya magharib A na B na Wilaya ya
Mjini ikiwemo Daraja bovu,Kinuni,Chumbuni,Fuoni na Mtoni kidatu.
Kaimu waziri amesema jumla ya wagonjwa ishirini na tatu (23)
wameripotiwa kuugua ugonjwa huo kutoka maeneo hayo tangu kuanza kwa
ugonjwa huo mwishoni mwa mwezi march mwaka huu.
Aidha amesema kutokana na kuibuka kwa maradhi ya matumbo na vimelea
vya ugonjwa wa kipindupindu wizara ya afya imewataka wafanya biashara
walioruhusiwa kufanya biashara zao kufuata taratibu za kiafya ili
kuepuka kusambaza vimelea hivyo kwa wateja wao.
![]() |
Nae mkurugenzi kinga na elimu ya afya Dk. Fadhil Muhammed amesema
mbali na kupiga marufuku vyakula vinavyouzwa kinyume na taratibu za
kiafya lakini pia si vyema kwa wananchi kuendelea na mikusanyiko wakati
wa futari hususan katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Jumla ya wagonjwa Efu 4 mia 3 na 30 waliugua ugonjwa wa kipindu pindu
kati yao 68 walipoteza maisha katika kipindi cha mwaka 2016 ,ambapo kwa
mwaka 2017 jumla ya wagonjwa 23 wameanza kuugua ugonjwa huo.
chanzo:Zanzibar24.
Comments