Hong ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Viettel, alifikishwa
mahakamani hapo jana pamoja na washitakiwa Dilshad Ahmed (36), Rohail
Yaqoob(47), Khalid Mahmood (59), Ashfaq Ahmad (38), Muhamad Aneess(48),
Imtiaz Ammar (33) wote raia wa Pakistan na Ramesh Kandasamy (36) raia wa
Sri-Lanka wanaokabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi.
Wakili wa Serikali, Jehovanes Zacharia alidai jana mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa washitakiwa Ahmed, Yaqoob, Mahamood,
Ahmad, Anees, Kandasamy na Qammar, Novemba mwaka jana Dar es Salaam
walikula njama kutenda kosa la kutumia vifaa vya mitandao.
Alidai kati ya Novemba mwaka jana na Februari mwaka huu, jijini Dar
es Salaam, washitakiwa hao walitengeneza mfumo wa kutumia huduma za
mtandao ili kukwepa kodi ya kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila
kibali cha TCRA.
Zacharia alidai washitakiwa katika kipindi hicho waliendesha hiyo
mifumo ya kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila ya kuwa na leseni.
Alidai Novemba 20, mwaka jana, washitakiwa hao waliingiza vifaa vya
kielektroniki bila ya kuwa na leseni na kwamba katika tarehe
isiyofahamika Novemba mwaka huohuo walisimika vifaa hivyo ikiwamo sim
box yenye namba ya siri 1152000.8.n.t.n na Laptop mbili aina ya Dell
bila ya kuwa na kibali cha TCRA.
Katika kipindi hicho, washtakiwa hao wanadaiwa kuunganisha vifaa
hivyo na huduma za mitandao ili kupokea na kusambaza mawasiliano bila ya
kuthibitishwa na TCRA.
CHANZO:hABARILEO.
Comments