
Akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Rahaleo amesema
kuelekea kwenye uzinduzi wa kampeni ya mimi na wewe itakayo anza kesho
kwa matembezi ya amani na kufuatiliwa na uchangiaji wa damu salama,
kutakua na zoezi la ujenzi wa madarasa 52 yaliyopo katika ngazi
mbalimbali zikiwemo za msingi, kozi nne na paa yatakamilika ili
kuwawezesha watoto wa mkoa huo kusoma katika mazingira mazuri.
Akizungumzia swala la uchangiaji damu salama amesema zoezi hilo
limekusudia kupunguza upungufu wa tatizo la damu kwa wagonjwa
wanaohitaji huduma hiyo hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa
ramadhani .
Hata hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi hapo kesho katika
harakati mbalimbali zitakazo fanyika ili kuipa sapoti serikali katika
hatua zake za kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka na kusema kuwa
kampeni ya mimi na wewe inalenga kuwarejesha wananchi katika uzalendo wa
kizanzibar na kuwachana na ubaguzi ambao unaleta mifarakano katika
jamii.
Aidha amesema baada ya kukamilika kwa kazi zote zilizokusudiwa katika
kampeni hiyo pia kutakuwa na uchangiaji wa vitu mbalimba kwa viongozi
ambapo vitu hivyo viwasaidia makundi mbalimbali wakiwemo wasio
jiweza,wazee mayatima,kaya maskini pamoja na watu wenye ulemavu.
Kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa na Makamo wa Rais Samia Suluhu
Hassan hapo kesho katika viwanja vya mnara wa kumbukumbu Mapinduzi
Squea kisonge.
chanzo:Zanzibar24
Comments