JPM ateua mkurugenzi wa TIC, RAS Morogoro.



Rais John Magufuli 
Rais John Magufuli leo (Jumatano) amemteua Geoffrey Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Kabla ya uteuzi huo Mwambe alikuwa mkuu wa wilaya ya Manyoni. Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni itajazwa baadaye.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Clifford Tandari kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro.
Tandari anachukua nafasi ya Dk  John Ndunguru ambaye amestaafu.
Kabla ya uteuzi huo  Tandari alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Uteuzi huo unaanza mara moja.
chanzo:Mwananchi.

Comments