Lukuvi alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ubungo, Saeed
Kubenea (Chadema) aliyetaka kujua ni lini baadhi ya maeneo ya Dar es
Salaam yatapimwa na wamiliki wake kupewa hati.
“Dar es Salaam haipimwi kwa sasa na hata huko Kimara hakupimwi ila
tunachofanya ni kurasimisha makazi ili wananchi wapate hati,miundombinu
iimarishwe na makazi yao kuongezewa thamani ili nyumba zao
ziwasaidie,”alisema.
Katika swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Kibamba,John
Mnyika(Chadema)akitaka kufahamu maeneo gani katika jimbo la Kibamba
hayajapimwa na lini yatapimwa pamoja na mpango wa kupunguza gharama na
muda waupimaji na utoaji wa hati ili kurahisisha na kuharakisha
upatikanaji wa huduma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani Jafo alisema
katika eneo la kata ya Kimara upimaji unaendelea na tayari viwanja 3,196
vimeshapimwa. Alisema taratibu zinakamilishwa ili kuwapimia wananchi
186 waliolipia gharama katika kata ya Kibamba ambao utahusisha upimaji
wa maeneo ya huduma za umma 123 katika Manispaa ya Ubungo.
“Upimaji umepangwa kufanyika katika kata za Mbezi, Msigani, Goba na
Kwembe kupitia kampuni binafsi zilizoidhinishwa na serikali ili
kuharakisha hilo,” alisema. Alitaja maeneo ambayo bado hayajapimwa ni
Kata za Manzese na Mabibo, Mburahati, Kimara, Saranga, Goba,Mbezi
,Kibamba ,Kwembe na Makuburi.
chanzo:Habarileo.
Comments