
Rais Duterte alisema kuwa hawezi kutoa ahadi yoyote ya kusafiri
kuenda Marekani kutokana na shughuli nyingi na safari anazopanga kufanya
nchini Urusi na Israel.
Bwana Trump alimpa mwaliko Duterte wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu kati ya wawili hao siku ya Jumamosi.
Rais huyo wa Ufilipo alikuwa amesrma kuwa yuko tayari kuboresha uhusiano na Marekani.
Alisema
kuwa tofauti zake na Marekani zilikuwa wakati wa kipindi cha Rais
Barack Obama ambaye wakati mmoja alimuita kuwa mtoto wa kahaba.
Wakati wa mawasiliano viongozi hao wawilia walizungumzia vita vyenye
utata dhidi ya madawa ya kulevya vinavyoongozwa na Rais Duterte ambavyo
vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 7000 chini ya mwaka mmoja.
Suala la Korea Kaskazini nalo liliibuka.
Ziara hiyo itakuwa fursa ya kujadili umuhimu wa ushirikiano kati ya Marekani na Ufilipino ambao kwa sasa unakua mzuri.
Mkutano kati ya Bwana Duterte na Obama ulifutwa baada ya Durtete kumtukana Obama.
chanzo:Bbc.
Comments