
Taarifa hiyo ilitolewa kwa vyombo vya habari hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala,
Simon Berege wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Alisema hayo baada ya kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo, kilicholenga kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo.
Alisema “wanyama hao wakiingia vijijini wanatishia sana maisha ya wananchi hasa wanawake na watoto, japo kuwa hawa wanawaogopa wanaume hivyo kwa ruhusa ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya tumeanzisha oparesheni maalumu ya kuwatokomeza fisi kwa kuwaua kwa kutumia bunduki na sumu,”
Alisema wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake, fisi mmoja tayari alikuwa ameuawa na maofisa wa idara ya wanyamapori katika Kata ya Chela, baada ya kutaka kutafuna watoto. Aliswema fisi waliouawa hadi sasa ni 14. Akifafanua juu ya idadi ya fisi waliouawa ili kunusuru wananchi kuliwa na fisi hao, mkurugenzi huyo alisema katika Kijiji cha Kakola waliuawa fisi saba, Kata ya Ngaya fisi sita na Kata ya Chela aliuawa fisi mmoja.
chanzo:zanzibar24.
Comments