Familia 2,603 zalipwa bil 7.4/- kupisha bwawa la Kidunda.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isaack KamwelweSERIKALI imeshalipa Sh bilioni 7.4 kwa familia 2,603 kama fidia ya kupisha ujenzi wa Bwawa la Kidunda lililopo katika kata ya Serembala Kiganila Mkoani Morogoro. Bwawa la Kidunda linajengwa mahususi kwa ajili ya kuhifadhi maji ya matumizi ya majumbani kwa wakazi wa Kibaha,Bagamoyo na Dar es Salaam.

Bwawa hilo halitahusu kilimo kikubwa cha umwagiliaji kwani serikali itaangalia uwezekano mwingine wa kuweka miundombinu wezeshi ya kilimo cha umwagiliaji kulingana na maeneo husika.


Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isaack Kamwelwe alisemaSerikali imetenga Sh bilioni 1.5 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na imepanga kutenga Sh bilioni mbili kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya fidia kulingana na tathmini iliyofanywa.

“Serikali inaandaa malipo ya fidia kwa mujibu wa sheria yaardhi ya mwaka 1999 ambayo inaelekeza pia kuwa endapo malipo ya fidia yatachelewa kulipwa kwa zaidi ya miezi sita tangu kupitishwa, mlipaji atapaswakufanya mapitio na kulipa nyongeza na muda uliozidi,”alisema.

Kamwelwe alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Prosper Mbena(CCM) aliyetaka kufahamu kama serikaliipo tayari kuboresha malipo ya fidia kwa wanavijiji wote walioathirika kwa nyumba na mashamba yao kuchukuliwa kupisha ujenzi wa bwawa la maji Kidunda nakama serikali ipo tayari kwenye bajeti hii kumalizia malipo ya takriban Sh bilioni 3.7 kuwafidia wananchi hao kulingana na tathmini iliyofanyika.
chanzo:habarileo.

Comments