
Amesema ingekuwa "heshima kuu kwake".
"Kungelikuwa na hali
mahsusi kwangu kukutana naye, ningekutana naye - bila shaka. Ingekuwa
heshima kuu kwangu kufanya hivyo," Bw Trump aliambia shirika la habari
la Bloomberg Jumatano.
Jumapili, alikuwa amemweleza Bw Kim kama "kijana mwerevu".
Tamko la Bw Trump limetokea huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Ikulu
ya White House baadaye ilitoa taarifa kufafanua matamshi ya Bw Trump na
kusema Korea Kaskazini ingehitaji kutimisha masharti mengi kabla ya
mkutano kati ya viongozi hao wawili kufanyika.

"Ni wazi kwamba kwa sasa, hakuna mazingira mahsusi (ya kufanikisha mkutano kama huo)," aliongeza.
Kwenye mahojiano na CBS Jumapili, Rais Trump alisema Bw Kim
alichukua mamlaka akiwa na umri mdogo, licha ya kukabiliana na "watu
wagumu na hatari sana."
Alisema hajui iwapo Bw Kim ana akili timamu.
Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini aliamrisha mjomba wake auawe miaka miwili baada yake kuingia madarakani.
Aidha, anatuhumiwa kuamuru kuuawa kwa ndugu wake wa kambo.
"Watu wanajiuliza: 'Je, ana akili timamu?' Sijui
mimi...lakini alikuwa kijana wa miaka 26 au 27...pale babake alipofariki
dunia. Bila shaka amekuwa akikabiliana na watu wakali na wagumu, hasa
majenerali wa taifa hilo na wengine.
"Na akiwa an umri mdogo hiyo,
aliweza kudhibiti madaraka. Watu wengi, nina uhakika, walijaribu
kumpokonya madaraka, iwe mjomba wake au watu wengine. Na alifanikiwa
kuchukua na kuyadhibiti madaraka hayo. Kwa hivyo, bila shaka, ni kijana
mwerevu."
Jumamosi, Korea Kaskazini ilifanya jaribio la kurusha kombora la
masafa marefu ambalo lilifeli, mara ya pili kwa jaribio kama hilo
kutekelezwa na Pyongyang katika kipindi cha wiki mbili.
Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka siku za karibuni, huku Korea Kaskazini na Kusini zikifanya amzoezi ya kijeshi.

Jumapili, makala katika shirika la habari la
serikali ya Korea Kusini KCNA ilitoa wito kwa Marekani kutafakari
kuhusu "madhara makubwa ambayo yanaweza kusababisha na uchokozi wake wa
kipumbavu wa kijeshi."
Korea
Kaskazini imekuwa ikifanya majaribio ya makombora mara kwa mara miezi
ya karibu na imekuwa ikitishia kufanya jaribio la silaha za nyuklia kwa
mara ya sita.
Rais Trump aliambia CBS kuwa Marekani "haitakuwa na furaha sana" iwapo majaribio zaidi yatatekelezwa na Korea Kaskazini.

chanzo:Bbc.
Comments