Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohammed Shein amesema kuongezwa kwa mishahara kwa wafanyakazi wa serikalini isiwe sababu kwa wafanyabiashara kuongeza bei bidhaa zao kwani kutaongeza maisha ya wananchi hasa wasio wa serikali kuwa na maisha magumu.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi dunia amesema wafanyabiasha kuoandisha bei bidhaa kiholela sijambo jema kwa wananchi na serikali haitambui kabisa ongezeko hilo ambalo halipo kisheria na kuwacha mara moja hasa kipindi hichi cha kuendea Mwezi mtukiufu wa Ramadhani.
Akizungumzia haki za wafanyakazi amesema atahakikisha anawajengea mazingira bora wafanyakazi wote wa serikali na sekta binafsi kujengewa maslahi mazuri ya mishahara ili na wao waweze kufaidika na kuweza kufanyakazi kwa bidii licha ya changamoto wanazokabiliana nazo.
Dokta Shein ametoa onyo kwa wafanyakazi wasiojali kanuni za kazi,wababaishaji,wababe na wasio na nidhamu kazi kuwa watawajibishwa na hata kufukuza kazini kutokana na vitendo vyao visivyoleta tija katika taasisi.
Kwaupande wao Viongozi wa nyama vya wafanyakazi na Waajiri Mkurugenzi Zanema Salaah Salum Salaah na Mwenyekiti wa waajiri Khamis Mwinyi Mohamed wamesema kwa kipindi kirefu wafanyakazi wanasisitiza kuimarishwa kwa masilahi kwa wafanyakazi,Kupunguzwa kwa kodi na mishahara duni na kubwa ni kupatikana kwa haki na maslahi bora kwani uchumi wa taifa utategemea wafanyakazi hivyo haki zao zilindwe ili wawajibike.
Siku ya wafanyakazi huadhimishwa kila mwaka ifikapo Mai mosi ambapo ujumbe wa mwaka huu ni Uchumi wa taifa unatengemea wafanyakazi,hali zao zilindwe ili wawajibike.
chanzo:Zanzibar24
Comments