Dk Asha Rose Migiro: Hakuna mtanzania aliyeathirika katika shambulio la Manchester nchini Uingereza.

Balozi Dk Migiro alimweleza mwandishi wetu kwamba taarifa juu ya
tukio hilo la kusikitisha bado zinaendelea kukusanywa na kwamba Waziri
Mkuu wa Uingereza anakutana asubuhi hii na Kamati ya Masuala ya Usalama
na Maafa kupata tathmini ya tukio na hatimaye kulitolea taarifa rasmi.
Mpaka sasa haijafahamika nani wanahusika na utekelezaji wa tukio hilo
lakini inasemekana limefanywa na mtu aliyejitolea mhanga na kwamba
muhusika pia ni mmoja wa watu walikufa katika mlipuko huo.
Balozi Migiro imeleelezea masikitiko yake juu ya tukio hilo na kutoa
wito kwa yeyote mwenye taarifa zaidi kuwasiliana na ofisi ya Ubalozi.
chanzo:zanzibar24.
Comments