
Jeshi la Polisi katika mkoa wa kipolisi Ilala limethibitisha kutokea
kwa tukio hilo, lililofanyika katika nyumba ya mwajiri wa dada huyo wa
kazi, ambapo mpaka sasa haijafamika chanzo cha dada huyo kujiua.
Mwajiri wa binti huyo, Anna Kasanda alisema alipokea taarifa saa 9:00
alasiri kwamba kuna tatizo nyumbani kwake, na ndipo alipoamua kurudi
nyumbani na kukuta mfanyakazi huyo amejiua.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
chanzo: zanzibar24.
Comments