
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na Balozi Mdogo China Zanzibar Bw. Xie Xiaowu uliotembelea Afisi Kuu Kisiwandui Zanzibar.
Amesema ushirikiano uliopo baina ya vyama na serikali za nchi hizo
zimeimarika na kuzaa matunda yanayowanufaisha wananchi wa pande zote
mbili katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Dkt. Mabodi alieleza kwamba njia pekee ya kulinda hazina hiyo ni
kuwarithisha Vijana Elimu na ujuzi zitakazowasaidia kupata uwezo wa
kitaaluma wa kulinda urithi huo dhidi ya maadui na wapinga maendeleo wa
nchi hizo.
“ Ushirikiano baina ya CPC na CCM ni ya muda mrefu hivyo sisi vizazi
vya sasa ni lazima tujivunie huku tukiyalinda ili tuendele kunufaika na
fursa za nchi hizo.
Kwa upande wake Balozi Mdogo wa China Bw. XIE XIAOWU ameahidi kwamba
China itatoa ushirikiano wa Ari na Mali ili kuhakikisha Zanzibar inakuwa
nchi yenye nguvu kiuchumi na kijamii.
Alisema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha mahusiano baina ya vyama
hivyo na serikali zake ili viweze kutekeleza kwa ufanisi mikakati ya
kimaendeleo iliyoachwa na Viongozi Wakuu wa taasisi hizo toka enzi za
kusaka uhuru wa nchini hizo.
Sambamba na hayo Balozi huyo Bw. Xie Xiaowu alisifu juhudi za
maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayotokana
na CCM kuwa zinaongeza ushawishi na nia ya China kuendelea kusaidia
sekta mbali mbali nchini ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Pamoja na Hayo alimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.
Mabodi kuwa ni kiongozi mchapakazi kutokana na kuwa karibu na taasisi za
kimataifa pamoja na wananchi kwa ujumla licha ya kuteuliwa kushika
nafasi hiyo kwa muda mfupi.
“ China inathamini juhudi mikakati mbali mbali ya maendeleo
inayofanywa na Serikali ya Mapinduzi kwa lengo la kutekeleza Ilani ya
Uchaguzi ya Chama Tawala, hivyo na sisi bado tuna nia na mikakati ya
muda mrefu ya kuwaunga mkono kupitia sekta za Afya, Elimu, Uvuvi na
Miundombinu”, alifafanua Balozi huyo wa China.
Baada ya ziara hiyo Ujumbe wa China ulitembelea sehemu mbali mbali za
makumbusho zikiwemo sehemu aliyouliwa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa
Zanzibar na mwenyekiti wa balaza la mapinduzi Marehemu Mzee Abeid Karume
kisiwa ndui mjini zanzibar.
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Balozi mdogo wa China Zanzibar Bw. Xie Xiaowu pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo la CCM Kisiwandui Zanzibar. PICHA NA AFISI KUU ZANZIBAR. |
CHANZO:ZANZIBAR24.
Comments