Alitoa kauli hiyo juzi wakati wa ziara yake ya kukagua miradi
mbalimbali katika kata ya Kibaigwa, ikiwemo ujenzi wa chumba cha
upasuaji katika Kituo cha Afya Kibaigwa, ukarabati wa soko la mboga na
matunda katika kata hiyo lenye takribani vibanda 800.
Kizigo ampongeza
Diwani wa Kata hiyo na uongozi wa CCM wa kata chini wa Katibu Kedmon
Chilongola kwa kusimamia na kuhangaikia matatizo ya wananchi kwa vitendo
na kusisitiza umoja kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya kata ya Kibaigwa.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015
diwani wa Kibaigwa, Richard Kapinye alibainisha kuwa walifadhiliwa fedha
kiasi cha Sh milioni 166.8 na Taasisi Local Investment Climate (LIC)
kwa ajili ya ukarabati wa soko hilo.
Alisema waliweza ukarabati banda la
kuuzia samaki, mchele, nyanya na banda la matunda, ujenzi wa choo
chenye matundu nane, vizimba viwili vya taka ngumu, ujenzi wa mabanda
mawili mapya ya kuuzia mboga, kuingiza umeme, mifereji ya kuzuia maji
kuingia katika soko hilo. Alisema maendeleo ya mradi huo kwa sasa ni
asilimia 92 na unatarajiwa kuzinduliwa wakati wa mbio za Mwenge wa
Uhuru, Juni 2017.
Kizigo alishuhudia ujenzi wa chumba cha upasuaji katika Kituo cha
Afya Kibaigwa unaogharimu Sh milioni 30 na sasa ujenzi upo hatua ya
kutandika jamvi na Katibu wa Kamati ya Ujenzi ambaye ni daktari mkuu wa
kituo hicho Shalua Mkumbo alisema baada ya wiki mbili ukuta wa jengo
hilo utakuwa umekamilika.
Kapinye alisema Kituo cha Afya Kibaigwa tayari
kimepata mashine ya kupimia magonjwa (Ultrasound) na Kampuni ya
Serengeti Brewerries Ltd imechimba kisima kirefu cha maji cha kutumia
umeme wa jua chenye thamani ya Sh milioni 83 katika zahanati ya
Kibaigwa.
Pia katika kijiji cha Ndurugumi kilichimbwa kisima cha maji
cha thamani ya Sh milioni 18 na ukarabati wa tangi kwa sasa eneo hilo
wameondokana na shida ya maji iliyokuwa ikiwakabili 2016/1017 na hadi
kufikia sasa katika kata hiyo kuna zaidi ya vichoteo 10 vya maji .
Aidha Kizigo alitembelea mradi wa choo uliokamilika katika shule ya
msingi Miembeni chenye matundu 16 uliojengwa kwa ufadhili wa Ubalozi wa
Afrika Kusini na kusisitiza kuwa serikali iliyopo madarakani ndio
inaunganisha ufadhili huo.
Kizigo amewasisitiza wajumbe wa Halmashauri
Kuu ya Kata hiyo kuhakikisha chama kinakuwa imara kwa kutunza siri za
chama na kuhakikisha wanapofanya uchaguzi kuchagua viongozi kuanzia
ngazi ya tawi wanaoelewa wapi Tanzania inapoelekea.
Kwa upande wao
wananchi wa kata hiyo wameipongeza serikali ya CCM kwa kuboresha huduma
za kijamii kwa kasi hususani kituo cha afya na mazingira ya soko kwani
wafanyabiashara wataongezaka.
chanzo:Habarileo.
Comments