CAR kukumbwa na mgogoro wa kiuchumi kwa kuondoka wanajeshi wa Uganda.

Eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati litakumbwa na mgogoro wa kiuchumi baada ya wanajeshi wa Uganda kuondoka katika eneo hilo. Wanajeshi hao wa UPDF walikuwa wametumwa nchini humo kupambana na waasi wa Kikristo wa LRA.

Duru za kuaminika za Jamhuri ya Afrika ya Kati zimetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, hatua ya kuwarejesha nyumbani wanajeshi 500 wa Uganda waliotumwa mashariki mwa nchi hiyo kutawasababishia matatizo ya kiusalama na kiuchumi wakazi wa eneo hilo. 


Operesheni ya kuwarejesha nyumbani wanajeshi wa Uganda waliotumwa kupambana na magaidi wa LRA huko Jamhuri ya Afrika ya Kati inamalizika mwishoni mwa mwezi huu wa Mei.

Duru hizo za Jamhuri ya Afrika ya Kati zimesema kuwa, viongozi wa mji wa Obo wa mashariki mwa nchi hiyo hawajawa na uwezo wa kulinda usalama wa maeneo hayo na kuna hatari mji huo ukakumbwa na mashambulizi ya waasi wa Kikristo wa LRA, baada ya kuondoka wanajeshi wa Uganda.

Ukiachana na masuala hayo ya kiusalama, kuweko wanajeshi wa Uganda huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kumekuza pia uchumi wa mji wa Obo hasa kwa vile wafanyabiashara wa mji huo walikuwa wakitoa bidhaa zao Sudan Kusini kutokana na kuweko usalama katika eneo hilo. 

Hata hivyo kuondoka wanajeshi wa UPDF mjini humo kutasababisha matatizo makubwa ya kiusalama na pia ya kiuchumi.

Ikumbukwe kuwa, mwaka 2009, wanajeshi wa UPDF wa Uganda walichukua jukumu la kulinda usalama wa wakazi 15 elfu wa mji wa Obo wa mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
chanzo: parstoday.

Comments