Bara bara yawatenganisha wananchi Kisiwani Pemba


Image may contain: tree, outdoor and natureAfisa mdhamini Wizara ya Mawasiliano na Miundo mbinu Pemba Mh Hamad Ahmed Baucha amesema kufuatia kukatika kwa bara bara ya changaweni mkoani Wizara yake imechukua juhudi za kukaratabati bara bara kongwe iliyo kua ikitumika zamani ilikupisha ukarabati  ile iliyo haribika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi amesema athar kubwa ya kukatika  kwa bara bara changaweni kumepelekea kusimama kwa harakati za mawasiliano ya usafirki kwa muda kutoka chake chake kwenda mkoani kisiwani hapa.


Amefahamisha kuwa wamefanya jitihada kubwa ya kurejesha mawasiliano hayo kwa kuikarabati bara bara kongwe ili wananchi wapate hudumu hiyo ilikupisha kukarabati pale ambapo kumetokea tatizo la kuigawa wilaya ya chake chake na mkoani.

Ameeleza kuwa kwa sasa wanaendelea kufanya tathmini ya kubaini ukubwa wa  uharibi uliotokana na kuharibika kwa bara bara hiyo kutokana na ukubwa ya atahar zenyewe.

Image may contain: tree, outdoor and natureAidha amewaomba wananchi kuendelea kuwa na ustahamilivu  huku serekali  kupitia wizara hiyo ikiendelea kuharakisha ukarabati ili huduma hiyo iweze kupatikana kwa muda muafaka.

Image may contain: tree, plant, shoes, sky, outdoor and nature

Comments