Auawa akigombea shamba, mwili wake wachomwa moto.

Mkazi wa kijiji cha Kisaki Kituoni wilayani Morogoro, Yusuph Lipewa (54) amefariki dunia baada ya kuuawa kisha mwili wake kuchomwa moto kufuatia ugomvi wa kugombea mipaka ya mashamba.
Mjomba wa marehemu, Msafiri Saidi (27) amesema kuwa marehemu alifikwa na mauti baada kupigwa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na mwili wake ukichomwa moto baada ya kipigo hicho.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukuo hilo Mei 15, mwaka huu saa 3.00 asubuhi  na kwamba jeshi hilo tayari linamshikilia mtuhumiwa  kutokana na mauaji hayo.
Matei amesema uchunguzi bado unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa  atafikishwa mahakamani.
chanzo:Mwananchi.

Comments