
Polisi wanasema kuwa mshukiwa anayejulikana kama Gangeshananda
Theerthapada alikuwa akizuru katika nyumba ya mwanamke huyo ili
kumfanyia matambiko ya ibada babake mwanamke huyo aliyekuwa mgonjwa.
Mamake alitumai kwamba jamaa huyo aliyejidai kuwa mtakatifu atandolea familia hiyo matatizo.
Badala yake ,mwanawe anasema alikuwa akimbaka kila anapotembea nyumba hiyo
Siku ya Ijumaa usiku, alichukua kisu na kumshambulia alipojaribu kumbaka na baadaye akaita maafisa wa polisi.
Mbakaji huyo baadaye alikimbizwa hadi katika taasisi ya elimu ya
matibabu ya Thiruvananthapuram ili kufanyiwa upasuaji wa dharura
Hopsitali hiyo ilisema katika taarifa : Mtu mwenye umri wa miaka 54 alilazwa katika hospitali hiyo siku ya Jumamosi.
”Asilimia 90 ya uume wake ulikuwa umekatwa na hakuna njia ya kuushona na kuurudisha mahala pake”.
Wapasuaiji katika hospitali hiyo walimfanyia upasuaji wa dharura ili
kuzuia damu iliokuwa ikimwagika na kumwezesha kupitisha mikojo.
chanzo: zanzibar24.
Comments