
Imedaiwa mahakamani hapo na muendesha mashtaka wa Polisi Omar Mohd
mbele ya Hakimu Muhammed Subeti kwamba siku ya tarehe 10 mwezi huu
majira ya saa 1o jioni mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakani hapo kwa kosa
la uvunjifu wa amani ambapo mtuhumiwa huyo alimfungia mlango mpangaji
wake Jamila Juma mkaazi wa Mkokotoni kwa madai ya kuwa anadaiwa kodi ya
chumba jambo ambalo ni kosa kisheria.
Kesi dhidi ya mtuhumiwa huyo imefunguliwa mahakamani hapo na baada ya
kusomewa kosa lake mtuhumiwa amekataa na kuiomba mahakama impe dhamana
jambo ambalo lililkubaliwa mahakamani hapo kwa masharti ya kujidhamini
yeye mwenyewe kwa vile ana mtoto mchanga na kesi yake kusikilizwa tena
tarehe 22 mwezi huu kwa upande wa mashahidi.
chanzo: zanzibar24.
Comments