Rais wa zamani wa Korea Kusini, Park Geun-Hye amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mjini Seoul kwa tuhuma za ufisadi.
Hii
ndio mara ya kwanza ameonekana hadharani tangu kuondolewa madarakani na
kuzuiliwa mwezi Machi mwaka huu. Amekanusha kufanya makosa yeyote.
Bi
Park alifika mahakamani akiandamana na rafiki wake wa karibu, Choi
Soon-Sil ambae anatuhumiwa kwa kujipatia fedha kutoka kwa makampuni
makubwa.
Alipofika mahakamani Park Guen-Hye aliulizwa ajira yake na kujibu hana hajaajiriwa.
Yeye
na rafiki wake huyo hawakuzungumziana na walikaa kando ya mawakili wao.
Rais huyo wa zamani alivalia mavazi meusi na siyo sare za wafungwa
ambazo amekua akivalia gerezani.
Alikua
pia na kibandiko cha nambari yake ya mfungwa 503. Nywele zake
zilifungwa kwa kipini kilichotolewa na mamlaka za gereza. Kwa sasa
kiongozi huyo anakumbwa na njiya panda baada ya kuondolewa kwenye ikulu.
chanzo:Bbc.
Comments