Al-Barakah Foundation Tanzania yatoa msaada kwa waathirika wa maafa ya mvua Pemba.

Jumuiya ya Al-Barakah Foundation Tanzania iliopo Mkoani Morogoro imekabidhi msaada  wa vyakula vya aina mbali mbali kwa waathirika wa maafa yaliyo sababishwa na mvua katika maeneo tofauti kisiwa cha Pemba.

Akikabidhi msaada huo mkurugenzi mipango wa jumuiya hiyo Mussa Ali Buruki amesema jumuiya hiyo imekuwa ikijishughulisha na masuala mbali mbali ya kijamii ikiwemo kujenga Miskiti pamoja na uchimbaji wa visima.


Akipokea msaada huo Afisini kwake Mkuu wa Mkoa  wa kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla ameitaka jumuiya hiyo kuendelea kuwa na  mshikamano kwani bado misaada zaidi inahitajika.

Kwa upande wao waathirika wa maafa hayo ambao walikabidhiwa msaada huo wameomba   kusaidiwa ujenzi wa nyumba zao ambazo zimeharibika vibaya na hata nyengine kuanguka kabisa.

Comments