Watu 35 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Ally’s lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Tabora kugongana uso kwa uso na Coaster iliyokuwa ikitoka Kahama kwenda Mwanza, katika kijiji cha Usanda halmashauri ya Shinyanga vijijini mkoani hapa.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Muliro Jumanne amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi la kampuni ya Ally's kuwa kwenye mwendo kasi.
Jumanne amesema kuwa abiria waliokuwa kwenye magari hayo ni zaidi ya 70 lakini waliojeruhiwa ni 35 ambao ndiyo wamelazwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk Rashid Mfaume amesema amepokea majeruhi 35 wa ajali hiyo wakiwemo watoto wawili na kwamba kati ya majeruhi hao wenye hali mbaya ni wawili,
chanzo:mwananchi.
Comments