Waziri Mwakyembe alitoa taarifa hiyo jana bungeni alipokuwa
anawasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 ya Sh
bilioni 28.2.
Kwa mujibu wa Waziri, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) ilifanya ukaguzi wa kina katika huduma za utangazaji kwa mwaka wa
fedha wa 2016/2017 ikihusisha ukaguzi wa vifaa vya utangazaji, vyumba
vya habari, maktaba, mikataba ya ajira pamoja na sifa za watangazaji
katika vyombo vya habari.
‘’Vituo vyote vimeonesha kuwa na ubora wa huduma inayotolewa, hata
hivyo asilimia 90 ya wafanyakazi wamebainika kutokuwa na sifa za
kitaaluma za uandishi wa habari na utangazaji na kwamba hiyo ndiyo
changamoto kubwa inayoikabili tasnia ya habari,’’ alisema Dk Mwakyembe.
Ukiacha changamoto hiyo, Waziri alisema taasisi zote zilizo chini ya
Wizara yake zimefanya vizuri katika majukumu yake kwa mwaka wa fedha
uliopita, miongoni mwake ni pamoja na Kampuni ya Magazeti ya Serikali
(TSN) wazalishaji wa magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo na
Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC).
Taasisi nyingine ni TCRA, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA),
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Dk Mwakyembe alitoa pongezi kwa TSN
kwa kuboresha majukumu yake ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha
na kuongeza kwamba kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 magazeti hayo ya
serikali yamevutia wasomaji wengi na pia kuongeza idadi ya watangazaji
katika magazeti hayo kiasi cha kuongoza katika matangazo kwenye vyombo
vya habari.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Juma
Nkamia aliipongeza serikali kwa kutenga Sh bilioni 2.4 kwa ajili ya
kununua mtambo mpya wa kisasa wa uchapishaji magazeti kwa ajili ya TSN.
“Kamati inapendekeza mtambo wa sasa wa kuchapisha magazeti wa Dar es
Salaam uhamishiwe makao makuu ya serikali Dodoma ili kurahisisha
usambazaji wa magazeti katika mikoa jirani ya Tabora, Mwanza, Iringa na
mikoa mingine
chanzo:habarileo.
Comments