
Akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya
Malaria Dunia katika ukumibi wa mikutano wa Wizara ya Afya Mnazimmoja,
amezitaja shehia hizo kuwa ni Tumbatu Jongowe, Miwani, Micheweni,
Chukwani na Kiwengwa.
Hata hivyo amesema maambukizi ya malaria katika maeneo hayo
yanasababishwa na wasafiri wanaoingia na kutoaka nje ya Zanzibar mara
kwa mara ambapo mwaka jana asilimia 55 ya wagonjwa waliogundulika
walikuwa na tabia hiyo.
Amesema takwimu za Malaria Zanzibar zinaonyesha mafanikio mazuri
ambapo mtu mmoja kati ya watu mia moja hupata ugonjwa huo katika jamii
isipokuwa shehia hizo tano.
Naibu Waziri wa Afya amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari
za kujikinga na Malaria ikiwemo kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa na
kusafisha mazingira kwa lengo la kuondosha mazalio ya mbu wanaoeneza
maradhi hayo.

Amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakikataa kupigiwa dawa nyumba
zao kwa madai kwamba zinawaletea athari za afya jambo ambalo halina
ukweli kwani dawa hiyo ni salama kwa afya.
Amekubusha kuwa Sheria ya Afya ya Jamii na Mazingira ya mwaka 2012
pamoja na mambo mengine inasisitiza juu ya udhibiti wa mbu na mazingira
hivyo wananchi watakaokataa kupigiwa dawa sheria itawabana.

Meneaja Kitengo cha kumaliza malaria Mwinyi Khamis alisema Zanzibar
imeweka mikakati ya kumaliza kabisa malaria ifikapo mwaka 2023 hivyo
juhudi za jamii na Wizara ya Afya ni muhimu.
Amesema mwaka jana watu watano walibainika kufa kwa malaria Zanzibar wakiwemo watoto wawili wenye umri chini ya miaka mitano.
Mapema akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Kinga na Elimu
ya Afya Dkt. Fadhil Mohd amewashauri wananchi wasikubali kula dawa ya
malaraia bila kupimwa na kuthibitishwa kuwa wanayo malaria.
chanzo:zanzibar24.
Comments