
Lengo kuu la Tathmini za aina hiyo kwa nchi ni kujua mafanikio
waliyopata na kasoro zinazowakabili ili kuweza kuimarisha utoaji huduma
kwa jamii.
Timu ya wataalamu wanaosimamia tathmini hiyo watatembelea sehemu
mbali mbali za Zanzibar na watafanya mahojiano na wataalamu, wafanyakazi
wa sekta mbali ikiwemo afya na wananchi wa kawaida ili kuona hali ya
utekeleza wa huduma za afya na sekta zinazochangia huduma hiyo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pemba Juma ambae ni Kaimu
Waziri wa Afya akifungua mkutano wa wataalamu hao katika Hoteli ya Ocena
View Kilimani, alisema Zanzibar imefarajika kufanyiwa tathmini hiyo.
Amesema kwa kipindi kirefu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imejiimarisha katika kuweka mikakati ya kuimarisha afya vijijini katika
Wilaya zote 11 na kujiweka tayari katika kupambana na majanga
yanapotokea.
Ameongeza kuwa kufuatia mikakati hiyo Zanzibar imeweza kufanya vizuri
katika zoezi la chanjo ya maradhi mbali mbali na kupata sifa kubwa
duniani katika kupambana na maradhi ya Malaria.
Amewahakikishia wajumbe hao kuwa taarifa naq mapendekezo watakayotowa
Serikali itayafanyia kazi na kuwashirikisha wadau kutoka Wizara na
Taasisi nyengine zinazogusa afya za wananchi.

Akitoa taarifa ya Shirika la Afya ulimwenguni (WHO) Mwakilishi wa
Shirika hilo Zanzibar Dkt. Ghirmany Andermichael alisema matokeo ya
tathmini hiyo itakuwa chachu ya hatua nyengine ya maendeleo katika
kuimarisha mpango wa Taifa katika usalama wa sekta ya afya Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib
amewahakikishia wataalamu wa kimataifa wanaosimamia Tathmini hiyo kuwa
Wizara itatoa kila ushirikiano na kuwa wawazi kutoa taarifa
wanazozihitaji kufanikisha kazi yao.
Amesema Wizara inaamini kuwa maradhi hayana mpaka yanaweza
kumshambulia mtu yoyote na wakati wowote bila taarifa hivyo wamekuwa
makini katika kujiandaa kupambana wakati wote.
chanzo: zanzibar24.
Comments