Wizara ya Habari kuanzisha mfuko wa maendeleo ya sanaa.



Naibu Waziri wa Wizara hiyo Anastazia Wambura
Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo ipo katika mchakato wa kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa ili kusaidia kuinua kipato na kuongeza tija kwa wasanii.

Ahadi hiyo ilitolewa bungeni  na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Anastazia Wambura wakati akijibu swali la mbunge wa Kinondoni Maulid Said Mtulia (CUF).
Mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani kwa kuwaongezea vijana ambao wameamua kujiajiri kwa nyimbo, maigizo na maonyesha ya mitindo ili kuongeza tija katika kazi zao.
 chanzo:Mwananchi.

Comments