
Afisa wa Afya kutoka kitengo cha malaria Mwinyi Issa Khamis amesema
chanjo hiyo inayofanyiwa majaribio na Shirika la afya Duniani ,katika
nchi tano za Africa ikiwemo Kenya ,Burundi na Malawi iwapo italeta
mafanikio itaweza kutumika Zanzibar katika kutokomeza ugonjwa hatari wa
Malaria.
Akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya malaria nchini amesema
wakati Zanzibar inasubiri matokeo ya Majaribio hayo kitengo cha kumaliza
maria kinafanya tathmini juu ya njia zitakazotumika kumaliza ugonjwa wa
malaria nchini.
Nae Naibu waziri wa Afya Zanzibar Harusi Saidi Suleiman amesema
Zanzibar tayari imekuwa na mulekeo mazuri wakumaliza malaria na tayari
imesha anzishwa sheria maalumu itayowabana watu wote ambao wanapuuza
taratibu za kiafya juu ya kujinga na kutokomeza ugonjwa huo.
Aidha amesema Wizara ya afya imekusudia kuwafikisha mahakamani
wananchi wanaopinga juhudi za serikali katika kutokomeza Malaria
wakiwemo wananchi wanaokataa kupigiwa dawa bila sababu za Msingi.
Katika kipindi cha mwaka jana watu watano wamefariki dunia kutokana
na kuugua Ugonjwa hatari wa malaria kati ya Watu waliougua ugonjwa huo.
chanzo:Zanzibar24.
Comments