Taarifa iliyotolewa na WFP imeashiria kuwa katika shambulio la hivi karibuni la watu wenye silaha katika mji wa Wau magharibi mwa Sudan Kusini raia wasiopungua 16 pia wameuawa na kusisitiza kwamba shirika hilo lina wasiwasi kutokana na machafuko na umwagaji damu unaoendelea kushuhudiwa nchini humo.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani vilevile limeeleza masikitiko yake kwa kuuliwa watu ambao wanafanya jitihada kwa ajili ya kuawasaidia mamilioni ya raia wa Sudan Kusini na kutaka maisha ya watu hao yalindwe.
Taarifa ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa watu wapatao elfu nane wakaazi wa mji wa Wau wamelazimika kuzihama nyumba na makazi yao na kuwa wakimbizi kutokana na kuendelea mapigano na machafuko katika mji huo.
chanzo:parstoday.
Comments