Rais John Magufuli, leo anatarajiwa kupokea taarifa ya kazi ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu imesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki ndiye atawasilisha taarifa hiyo kwa Rais.
Comments