Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu amesema Wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni wasifukuzwe bali waendelee na masomo ili kufikia malengo yao.
Msisitizo huo umetolewa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa masuala ya kijinsia ulioandiliwa na Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu(DUCE).
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha DUCE, Profesa William Anangisye amesema lengo la mkutano huo ni kuleta chachu ya kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kupata wanasayansi wanawake nchini.
chanzo:zanzibar24.
Comments