
Mpaka sasa upinzani umegawanyika pande mbili, ukiwemo ule unapinga
kuteuliwa kwa Felix Tshekedi licha ya kuongoza kundi kubwa na upande
mwingine ni wanaomuunga aliyekuwa mshauri mkuu wa marehemu Tsichekedi
ambaye alifukuzwa kwenye chama hicho, baada ya kufanya mazungumzo na
Rais Kabila.
Hata hivyo kwa mujibu wa rais kabila, kuteuliwa kwa waziri mkuu
mpya ni kutatatua mvutano uliozuka, kuhusi utekelezaji wa makubaliano ya
tarehe 31 Desemba mwaka jana, makubalino ambayo yanataka waziri mkuu
atoke upande wa Muungano wa upinzani, lakini hadi sasa bado hawaja
afikiana kuhusu namna ya kufanya uteuzi, kutokana na mgawanyiko ulitokea
upande huo wa upinzani baada ya kifo cha marehemu mkogwe wa upinzani
Etienne Tshisekedi, ambae alikuwa anaongoza muungano huu, licha mtoto
wake kuteuliwa kuchukuwa nafasi yake hiyo.
chanzo:Bbc.
Comments