
Imedaiwa na Muendesha Mashtaka khalid Daud mbele ya hakimu muhammed
thubeit kwamba siku ya jumatatu ya tarehe 17/ 4 mwakwa huu majira ya saa
11 alfajiri huko Nungwi Wilaya ya Kaskazi A katika baa ya Coco bero
watuhumiwa hao walipigana hadharani na kusababishiana majeraha huku
wakijua kwamba jambo hilo ni kosa kisheria.
Mtuhumiwa Abubakar Ramadhan yeye amejeruhiwa kwa kuchinjwa sehemu ya
shingoni na miguuni kwa upande wa bi Engel yeye amejeruhiwa kwa
kuchinjwa mkono wake wa kulia.
Baada ya kupandishwa mahakamani watuhumiwa hao wote walikataa na
kuiomba mahakam iwape dhamana jambo ambalo lilikubaliwa kwa mashariti ya
kila mmoja awe na wadhamini 2 na barua za sheha zinazoonesha namba za
nyumba na vitambulisho vya mzanzibari masharti ambayo yaliwashinda.
hivyo mahakama hiyo imewarudisha rumande watuhumiwa hao na kusubiri hadi tarehe 24 mwezi huu kesi yao itakapotajwa tena.
chanzo: zanzibar24.
Comments